Duration 5:40

Sizonje - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro (Official Video)

981 964 watched
0
4.5 K
Published 5 Mar 2016

Nyimbo Mpya ya Mwaka 2016, Sizonje. [Kibwagizo – Banana Zorro] Sizonje hii ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Sizonje ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu [Bridge – Banana Zorro] Tulikaa barazani, tukasikia kelele Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani Sizonje, karibu nyumbani kwetu Uone maajabu ya nyumba yetu [Verse 1 – Mrisho Mpoto] Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu, Tulipoficha mundu za kupondea wezi, Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya? Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne, Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango, Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili, Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea, Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni, Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako Wanashangaa mbona ghafla Samahani sana mgeni Wapishi wameniomba kwamba Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba Eti unapenda vya mafuta au vya nazi? Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje Sizonje chumba hiki naomba usiingie Ukimaliza nitakwambia kwanini Kuna sauti inajirudia mara kwa mara Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa “USIYEMTAKA KAJA” Hatukuwahi kuelewa maana yake Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia [Chorus – Banana Zorro] Sizonje hii ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Sizonje hii ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu [Verse 2 – Mrisho Mpoto] Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto Na kamwe mtoto hawezi kuungua Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi Njoo huku uone Sizonje Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue? Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua Lile pale ni shimo la taka Na kile pale ni choo Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka Wala kwenda chooni Kama ukiwa makini Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi “KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?” Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje Kuna watoto, wazee na kina mama Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele Ninavyosikia, ila sina uhakika Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni Uone maajabu mengine ya nyumba hii Sizonje, ukiona tembo anaringa Ujue mvua zinakaribia [Chorus – Banana Zorro] Sizonje hii ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Sizonje ndio nyumba yetu Milango ipo wanapita madirishani Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Category

Show more

Comments - 389