Duration 4:17

TASWIRA KIMATAIFA : Mzozo wa Bwawa la Al Nahdha wapelekwa UN, Watu 500,000 wafa kwa korona duniani

82 watched
0
2
Published 1 Jul 2020

Mgogoro Wa Bwawa La Renaissance (Al Nahdha) Baina Ya Misri, Sudan Na Ethiopia Umewekwa Rasmi Kwenye Meza Ya Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Baada Ya Misri Kuwasilisha Mswada Huo Kwa Ajili Ya Kujadiliwa Na Wanachama Wa Baraza Hilo. Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Misri, Sameh Shoukry Amesema Nchi Yake Imewasilisha Faili Ya Mgogoro Wa Bwawa La Renaissance Kwenye Meza Ya Baraza La Usalama Kwa Ajili Ya Kujadiliwa Na Kwamba Hatua Hiyo Inaafikiana Na Matokeo Ya Kikao Cha Ofisi Ya Umoja Wa Afrika Kuhusiana Na Kadhia Hiyo. Kwingineko, Visa Vya Maambukizi Ya Virusi Vya Korona Duniani Vimepita Million 10 Sasa Huku Watu Zaidi Ya Laki Tano Wakiaga Dunia. Takwimu Za Sasa Zinaonesha Kuwa Watu 508,000 Wameaga Dunia Kutokana Na Virusi Hivyo Vilivyochipukia Mkoani Hubei Nchini Uchina Desemba Mwaka Jana, Kati Ya Visa Vya Maambukizi 10,430,000. Tafadhali Bonyeza SUBSCRIBE kupata uhondo zaidi #Taswira_Kimataifa #AlNahdha #CoronaVirus

Category

Show more

Comments - 0