Duration 1:40

Maajabu yatokea kaburi la maalim Seif , RC atoa onyo kwa wanao chukua mchanga

20 868 watched
0
85
Published 8 Mar 2021

FAMILIA ya aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad imesema baadhi ya wananchi wanaokwenda kuzuru kaburi wamekuwa wakichukua kwenye kaburi, hilo kwa madai kwamba unanukia hali ambayo inawapa wasiwasi juu ya matumizi ya mchanga huo. Kiongozi wa Familia hiyo Seif Ali Seif ambaye ni Mjomba wa Marehemu, ameiambia kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba kuwa vitendo hivyo amekuwa akivikemea kwani hajui mchanga huo wanaenda kuutumia kwa shughuli gani. Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi Salama Mbarouk Khatib amewataka wananchi wanaokwenda kuzuru kaburi hilo kuacha tabia ya kuchukua mchanga bali wafanye shughuli za kumuombe dua na sivyenginevyo. Pemba ACP Juma Sadi Khamis ameahidi kumchukulia hatua mwanachi ambaye atabainika kuhusika na kitendo hicho huku na Shekhe Omar Hamad naye amewataka wananchi kujiepusha na tabia hiyo. #UGATvFurahaYako

Category

Show more

Comments - 43