Duration 4:53

MKANDARASI ALIYEHATARISHA USALAMA KWA KUWEKA EARTH FEKI HATIMA YAKE HII

147 watched
0
0
Published 21 Dec 2021

WAZIRI WA NISHATI AIAGIZA REA KUWACHUKULIA HATUA WAKANDARASI WADANGANYIFU KWENYE MIRADI YA UMEME KWANI WANAHATARISHA MAISHA YA WATUMIAJI WA UMEME. Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma. WAZIRI wa Nishati,January Makamba ameuagiza Wakala wa nishati Vijijini REA kuwachukulia hatua wakandarasi wadanganyifu kwenye miradi pamoja na kuwaondoa kwenye orodha ya wakandarasi wanaofanya nao kazi na kutowapa tena zabuni za kazi hizo kwani wanahatarisha usalama wa maisha. Waziri Makamba ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati wa kikao na Wafanyakazi wa REA,ikiwa ni siku chache baada ya Mkandarasi mmoja mkoani Njombe kubainika akiunganisha waya bandia wa kuzuia radi huku akisema kukatika kwa umeme kunasababishwa na ubora wa chini ya utekelezaji miradi. Sanjari na hilo ameutaka uongozi wa REA kuhakikisha wanasimamia kwa uamkini mkubwa miradi ambayo inatekelezwa na wakala huo kupitia wakandarasi. Aidha amefafanua kuwa ili REA iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa ni lazima wawe na idara ya Sera,Mipango na utafiti huku akisema Serikali imepanga kufikisha umeme katika vitongoji 37 elfu nchini vilivyobakia katika kipindi cha Miaka minne ijayo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini,Mhandisi Hassan Saidy akaeleza mikakati mbalimbali wanayoitekeleza huku Mwenyekiti wa Bodi ya REA Wakili Julius Kalolo akibainisha vyanzo vya mapato katika utekelezaji wa miradi ya REA. Kila Mwaka watanzania 22,000 hupoteza maisha kutokana na magonjwa ya kupumua yatokanayo na uvutaji moshi majumbani mwao kwa sababu ya shughuli mbalimbali zitokanazo na nishati ikiwemo kupika kwakutumia kuni . USISAHAU KU SUBSCRIBE CHANNEL YETU ILI UWE UNAPATA UPDATE MPYA KILA TUNAPO WEKA HABARI MPYA WAKATI WOWOTE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE MAANDISHI YA BLUU /channel/UCcCo ... https://www.instagram.com/kahamatvonline/ #KAHAMATVONLINE #HABARIZAHIVIPUNDE

Category

Show more

Comments - 1