Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameagiza wizara na wasimamizi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka DART kujenga kituo cha daladala na magari madogo katika eneo la Kimara ili kuwezesha wakazi kunufaika vyema na mradi huo.