Duration 7:2

UJASIRI NA UBUNIFU UTAKULETEA MAFANIKIO

44 747 watched
0
637
Published 17 Apr 2019

Please watch: "FIKIA MALENGO YAKO KIRAHISI " /watch/AEB06hqV3uPV0 --~-- Kila mmoja anapenda kuwa na mafanikio katika maisha yake, lakini mafanikio hayaji tu bila kufanya juhudi ama jitihada za dhati. Leo tutaangalia ujasiri unavyomfanya mtu kubuni njia mbalimbali za mafanikio. Mojawapo ya njia inayoweza kukutoa hapo ulipo na kukupeleka katika hatua nyingine nzuri zaidi ni ubunifu. Mtu yeyote anayependa kuwa na mafanikio maishani, inambidi awe mbunifu katika nyanja mbalimbali ili kama yeye ni mfanyabiashara aweze kuteka soko kubwa. Unaweza kuwa mbunifu katika fani yoyote ile uliyonayo, ama kipaji ulichopewa na Mungu, kitakachokufanya uwe mtu tofauti katika maisha yako. Kama wewe ni mwalimu ambaye ni mbunifu wa kufundisha, maisha yako yatakuwa mazuri kwa sababu utasifika kwenye shule yako na sifa zako zitafika mbali hadi shule nyingine. Hali hiyo itakufanya utafutwe na shule nyingi, hivyo ni uamuzi wako kuchagua uende wapi. Ama utatafutwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali uweze kuwasaidia katika masomo yao ili waweze kufaulu mtihani, hapo wewe si yule wa zamani bali umekuwa mtu mwingine wa tofauti, kutokana na ubunifu wako. Kama wewe, una ofisi ya ushonaji na ukawa mbunifu mzuri wa mavazi, sifa zako zitafika mbali zaidi na watu wengi watakutafuta kwa ajili ya kuwabunia mavazi yao. Tayari utakuwa umeshajijengea jina, cha msingi ni kuongeza jitihada ili wale wateja wako usiwapoteze. Kama wewe ni mbunifu wa kupika chakula ama vitafunwa mbalimbali, utajulikana mtaani, kwenye ofisi ama kampuni mbalimbali na hata kutafutwa na watu kwa ajili ya shughuli zao za sherehe. Hiyo ni mifano michache sana, ambayo unaweza kujifunza. Si hiyo tu, bali unaweza kutumia uhandisi wako kwa kujenga nyumba nzuri, ukatumia uandishi wako kwa kuandika habari nzuri, ukatumia udaktari wako kutoa ushauri na kutibu vizuri wagonjwa unaowaoona. Tumia akili yako uliyopewa na Mungu, kwa kuwa mbunifu ili uweze kuwa na maisha mazuri. Binafsi ninaamini kuwa kila mmoja Mungu amempa kipaji ama akili kwa ajili ya kuwa mbunifu. Tatizo lililopo kwa watu wengi ni kukata tamaa. Wengi wamekuwa wakikatishwa tamaa na ndugu, jamaa ama marafiki zao. Na mara nyingi, wanaweza kufanya jambo na lisifanikiwe kama walivyofikiri matokeo yake, badala ya kutafuta ufumbuzi kwa nini hali hiyo imetokea, hukata tamaa na kuamini kuwa hawezi kufanya jambo lolote likafanikiwa labda aajiriwe tu. Inabidi tubadilike kimtazamo, kiakili na kifikra ili kila mmoja afurahie maisha yake aliyopangiwa na Mwenyezi Mungu hapa duniani. Hivyo, endapo unaamini jambo fulani haliwezekani, ndivyo itakavyokuwa. Lakini endapo unaamini kuwa jambo fulani linawezekana, akili yako italifanyia kazi na kutafuta njia ya kulifanikisha. Kuamini kuwa unaweza kufanya jambo, kunakufungulia milango zaidi ya kuwa mbunifu katika shughuli na maisha yako. Akili yako, itafungua njia ya mafanikio kama utaitumia vema. Na pia, kama unataka kuona njia ya kukutoa hapo ulipo, ondoa ukuta wa kuona kuwa haiwezekani, ndipo mafanikio yako yatakapoonekana. Mafanikio makubwa yanakwenda kwa mtu anayefikiri kuwa na maisha ya viwango kwa ajili yake na wengine. Ni vizuri pia kuboresha biashara zako ama shughuli zako unazozifanya kwa ajili ya kukupatia riziki, ili wengine waweze kufurahia huduma zako na kukutafuta. Pia unaweza kujijengea tabia ya kuwa na mazoea ya kufikiri mbinu mbalimbali za maendeleo kwa dakika 10 kila siku, kabla hujaanza kazi yoyote. Zoezi hilo, ni rahisi na kama utalizingatia utaona matokeo yake mazuri, ni vema kulizingatia. Kwa upande mwingine, utagundua kuwa, watu wote waliofanikiwa, hupenda kujishughulisha, si wavivu. Penda kujiuliza unatakiwa kufanya nini ili uzalishe zaidi? Ama uwe na maisha bora zaidi? Majibu ya maswali hayo ndiyo yatakayokufanya uongeze bidii zaidi. Na kwamba, ili uweze kuzalisha kitu chochote, unatakiwa uwe na malighafi. Katika kufikia uamuzi makini, malighafi ni mawazo na mapendekezo ya watu wengine. Kuwa makini, usipende sana kuhitimisha jambo lako, kwa mawazo ya wengine. Kwani mawazo ya wengine yanakusaidia kuchekecha mawazo yako mwenyewe kwa kuwa akili yako ina ubunifu. Ili ufanikiwe katika kampuni yako ama kiwanda chako, inakupasa ufanye utafiti wa kujua ubora wa bidhaa zako kwa wengine. Uliza maswali kuhusu ubora wa bidhaa zako, ukubwa wake, bei yake ama mwonekano wake kwa jamii uko vipi ili uweze kufanya maboresho pale inapotakiwa. Kuwasikiliza wengine, kunakufanya kukuwezesha kuboresha pale penye upungufu. Usiache ku SUBSCRIBE na kuniachia mawazo yako kwenye COMMENTS, LIKE na SHARE PIA kwa wengine. . NIFUATE MITANDAONI INSTAGRAM: https://www.instagram.com/ezdenjumanne/ TWITTER: https://www.twitter.com/ezdenjumanne FACEBOOK: https://www.facebook.com/ezdenjumanne LINKEDIN: https://www.linkedin.com/in/ezdenjumanne . For Business please send me an email ezdenjumanne@gmail.com Or leave a text/ Whatsapp :(+255)716235195 #Ujasiri #Ubunifu #EzdenJumanne

Category

Show more

Comments - 77
  • @
    @thegirl14055 years ago Shukraan brother kwa somo makini sana ubunifu ni kitu cha kipekee ujasili mali kuna ujasili na mali mpaka kupata mafanikio ni dhahiri kwamba mtu ameichanganua ahsante kaka uwepo wako unafaida kwa vijana allah akubariki. ...Expand 4
  • @
    @francismsangi32445 years ago Kweli kabisa, kila siku asubuhi ni lazima utenge mda kidogo kwa ajili ya afya yako ikiwa ni pamoja na mazoezi, very perfect. 2
  • @
    @aminaalid97453 years ago Allah akuzidishie elm zaid na ufafaham uzidi kutufungua kifikra
    shukran sana.
  • @
    @rahemahrahemah27195 years ago Shukran kaka ezden somo zr mashaallah, kweli ktk maisha ubunifu nikitu pekee ambacho kinaweza kukubadilisha pia ujasiri kwa chochote unachotaka kukifanya, allah bless you. 2
  • @
    @fridaynjenje9925 years ago Asante kaka eziden kwa mafundixho yako yamebadilixha maisha yangu. 2
  • @
    @rehemabonza45295 years ago Asante kaka. Niko pamoja na wewe na siku moja nitakupigia nikwambie mafanikio yangu, sasa hivi bado ila namiini. Naendelea kujifunza kupitia wewe. Amina.
  • @
    @shabannuru235 years ago Ahsante kaka ezden j nimeipenda sana nasaha zako. 3
  • @
    @tibayawaafrica2 years ago Shukran my brother kwa soma lenye hamasa kubwa sana katika jamii.
  • @
    @shammoha52975 years ago Wengi wetu tunasahau upesi. Asante kw kutukumbusha. Be blessed brother ezden. 1
  • @
    @dottnatt71105 years ago Shukran kaka najifunza mengi kupitia mafundisho yako.
    allah akuzidishie kila la kher.
  • @
    @lucaskadaraja30115 years ago Shukran sana kaka kwa kutujali kila siku huwa unaniongezea kitu kweny mind yang mungu akuzidishie zaid # ezden rocker man. 2
  • @
    @shemahabdallah32325 years ago Kutumia masaa ma2 kila asubuh kwa ajl ya afy yak kabla hujashk cm, very perfect. 1
  • @
    @maniamba_co_tz5 years ago Uko vizuri brother pia nashukuru kwa kupata mongozo wa njia bora ya kuishi.
  • @
    @amosiluyu4395 years ago Nmejifunza kitu hapo makini sana kak be blessed.
  • @
    @safimusa10115 years ago Asante kaka, unanipaga ujasili sana
    mungu akubariki.
  • @
    @rajabuibrahimu43385 years ago Tatzo kubwa lilipo ni kukata tamaa.
    lazma tubadilike kifikra.
    mungu akuweke uzidi kutupatia chakula cha akili. God bless you.
    4
  • @
    @blessibrahim20983 years ago Big up my brother sijawah jutia kufatilia kazi yako kila siku naingiza kitu kipya.
  • @
    @hamisimusaa16984 years ago Brother to support population of people to improve from ideal to says and motivation people in life is not easy and life is not loss. By h kitate property.
  • @
    @ramafrica90165 years ago Bro uko vizuri tunafurahi kwa elimu yako utupayo mungu azidivitu vikali tuweze. 1
  • @
    @khammykisenga13645 years ago Ahahaha that for your device. Ila nimecheka ulivyochapia. 1
  • @
    @muhsinsalum23055 years ago Kaka ezden ka ujumbe nikazuri saana, ila hako ka picha ka huyo mtu kamenitisha kinafsi. 3
  • @
    @hassansaidramadhan89405 years ago Brother napata madini mengi sana kutoka kwako, trust me nakukubali sana na napenda unachofanya natamani siku moja niwe kama wewe.
  • @
    @woltabenadi21845 years ago Kaka wenizaidi yakichwa umeletwa kwajili yetu kitabu auna kaka. 1
  • @
    @mohamedmiraj31174 years ago Ubunifu ndio kila kitu siku hizi ajira hakuna.
  • @
    @umtweve45015 years ago Kaka eiden jumanne. Ivi hichi kitu wengi huzungumzia ila inamaana ukifikilia jambo baya huja mapema kuliko ukifikiria jambo zuti eti sipendi ujinga huu . ...Expand
  • @
    @omaiim40145 years ago Nimejifunza mengi sana kaka umenifanya nisikate tamaa. 1
  • @
    @azizacleny86775 years ago Each one teach one thnk you sir mung akuweke uje uone kitu nachokifny kwaajil ya motivation zako. 1
  • @
    @hoseamuyungu91335 years ago Ndiyondiyoo sijutaagi kumaliza bando nikikusikiliza ww endelea ivoiv pamoja sn. 2
  • @
    @Pathro_Cavosia5 years ago Asante sana kwa hili but how am i got to be jasiri ikiwa sina ujasiri? 1
  • @
    @thegirl14055 years ago Shukraan brother kwa somo makini sana ubunifu ni kitu cha kipekee ujasili mali kuna ujasili na mali mpaka kupata mafanikio ni dhahiri kwamba mtu ameichanganua ahsante kaka uwepo wako unafaida kwa vijana allah akubariki. ...Expand 4
  • @
    @umtweve45015 years ago Kaka eiden jumanne. Ivi hichi kitu wengi huzungumzia ila inamaana ukifikilia jambo baya huja mapema kuliko ukifikiria jambo zuti eti sipendi ujinga huu . ...Expand