Duration 5:00

KANISA LA E.A.G.T LA TUMA SALAMU ZA RAMBI KWA RAIS MAGUFULI

76 watched
0
0
Published 27 Jul 2020

Kanisa la Evangelastic Assembies of God Tanzania(E.A.G.T), limeungana na Taifa kutoa salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuondokewa na Mzee Mpaka . Salam hizo zimetolewa leo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kanisa la Evangelastic Assembies of God Tanzania(E.A.G.T), Dkt.Brown Mwakipesile katika ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani hapo maeneo ya Mlimwa Jijini Dodoma. Dkt. Mwakipesile amesema kuwa wanaungana na watanzania katika kuomboleza msiba wa taifa na afrika nzima kwani Mzee mkapa alikuwa alama kubwa kwa taifa na mataifa ya Afrika. Dkt. Mwakipesile amesema kuwa Mzee Mkapa ataenziwa kwa ukweli na uwazi wa Taifa la Tanzania kwa kuwataka watanzania kufichua mambo yote yasiyo faha katika taifa na kutaka taifa lisonge mbele kwa ukweli na uwazi katika kuleta maendeleo. “Na kweli Mzee Mkapa alifanya kazi kubwa kwa taifa letu hivyo hatuna budi kuyaenzi yale yote aliofanya kwa taifa ili kwa maslai ya watanzania aliokuwa akiwaongoza”,ameeleza Dkt. Mwakipesile.

Category

Show more

Comments - 0